Viongozi wa Uamsho wadai polisi waliwafanyia ukatili

Written by makame silima <http://mzalendo.net/author/makame-silima>   //
22/08/2014  // 



Wanachama wa kundi la uamsho wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi
wakitoka wakiwa chini ya ulinzi wa Magereza walipofikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory
Na Tausi Ally, Mwananchi

Ijumaa,Agosti22 2014 saa 10:13 AM

Asema: “Waliotuhoji hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi
na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa watupu na kutupiga”

Dar es Salaam. Viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu
Zanzibar (Jumiki), akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) wameilalamikia
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa polisi “walitumia ushenzi na ukatili”
wakati wa kuwahoji.

Farid na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne likiwamo la
kuwaingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi, kusaidia na
kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.

Washtakiwa hao walitoa malalamiko hayo jana kwa Hakimu Mkazi, Hellen Liwa
muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kuiomba Mahakama
iwaruhusu washtakiwa saba kwenda polisi kuhojiwa kwa ajili ya upelelezi
zaidi.

Baada ya wakili huyo kuwasilisha ombi hilo, Sheikh Farid aliuliza:
“Wametuomba tena kwenda kuhojiwa? Kwanza waliotuhoji hawakutumia ustaarabu
wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa
watupu na kutupiga”.

Sheikh Farid alidai kuwa kiongozi Mkuu wa Jumuiya za Uamsho, Sheikh Mselem
Ali Mselem alimweleza watu hao walichomfanyia.

Hata hivyo, Hakimu Liwa alimwambia alimtaka kuzungumzia kile ambacho
amekiona siyo cha kusimuliwa.

Aliendelea kueleza: “Walipigwa na wala hawakupewa matibabu na watu
wameumizwa, utakuta wanakojoa damu wiki moja hadi mbili, tunaomba wafanyiwe
uchunguzi wa afya zao.”

Mshtakiwa Salum Ali aliiomba Mahakama kupeleka daktari mahabusu kwa madai
kuwa wanafanyiwa vitendo vya ‘kuingiliwa kinguvu’ na kuhoji kwa nini
wamekamatwa Zanzibar na kushtakiwa Bara wakati waliokamatwa Arusha
walishtakiwa hukohuko na hawakupelekwa Dar es Salaam au Zanzibar?

Akiendelea kutoa malalamiko yake, Sheikh Farid alidai kuwa wao wamekamatwa
kwa sababu hawautaki Muungano na kwamba huo ndiyo msingi wa kesi hiyo.

Baada ya kauli hiyo, Hakimu Liwa alisema: “Tupo kwenye mchakato wa Katiba
Mpya na masuala ya muungano yanatajwa mbona watu wanasema na hawakamatwi?”

Mara baada ya Hakimu Liwa kusema hayo, Sheikh Farid alidai ni kwa sababu wao
wanahubiri ukweli na watu wanaukubali.

Hakimu Liwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya
kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.
Katika kesi hiyo, Sheikh Farid na Jamal Nooridin Swalehe (38) waliunganishwa
na wenzao 18 mahakamani hapo.

Mbali na Sheikh Farid na Jamal, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka
hayo ni Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka,
Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim, Hamis Amour,
Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othman, Rashid Ally, Amir
Hamis, Kassim Salum na Said Shehe.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni, mwaka huu walipanga
njama ya kutenda makosa hayo na kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi.

Katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini, Sheikh Farid anadaiwa kuwa
aliwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda
makosa ya ugaidi.

Pia Sheikh Farid anadaiwa kuwa kwa makusudi na akijua kuwa anatenda kosa
alitoa msaada kwa watu hao kutenda vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria na
anadaiwa kuwa katika kipindi hicho akiwa anajua kuwa Sadick na Farah
wametenda makosa ya kigaidi, aliwahifadhi.

Chanzo Mwananchi 

                 Thé Mulindwas Communication Group
"With Yoweri Museveni, Ssabassajja and Dr. Kiiza Besigye, Uganda is in
anarchy"
                    Kuungana Mulindwa Mawasiliano Kikundi
"Pamoja na Yoweri Museveni, Ssabassajja na Dk. Kiiza Besigye, Uganda ni
katika machafuko"

 

_______________________________________________
Ugandanet mailing list
Ugandanet@kym.net
http://kym.net/mailman/listinfo/ugandanet

UGANDANET is generously hosted by INFOCOM http://www.infocom.co.ug/

All Archives can be found at http://www.mail-archive.com/ugandanet@kym.net/

The above comments and data are owned by whoever posted them (including 
attachments if any). The List's Host is not responsible for them in any way.
---------------------------------------

Reply via email to